• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  MAYELE ATOKEA BENCHI DRC YASHINDA 3-1 KUFUZU AFCON

  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele ametokea benchi dakika mbili na ushei za mwisho leo timu yake ya taifa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikishinda 3-1 dhidi ya Mauritania Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi katika mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Mayele aliingia dakika ya 88 kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la pili, Cédric Bakambu mshambuliaji wa Olympiakos ya Ugiriki kwenye mchezo ambao kocha Mfaransa, Sébastien Desabre hakumtumia beki wa Simba, Henock Inonga Baka 'Varane'.
  Mabao ya DRC yamefungwa na mshambuliaji wa Amiens SC ya Ufaransa, Gaël Kakuta dakika ya 37,  Bakambu dakika ya 42 na beki wa Besiktas ya Uturuki, Fuka-Arthur Masuaku dakika ya 67, wakati la Mauritani limefungwa na beki wa UTA Arad ya Romania, Yacoub Abeid dakika ya 55.
  Huu ni ushindi wa kwanza kwa DRC kwenye kundi hilo baada ya kufungwa mechi mbili za awali na Gabon na Sudan. Msimamo wa Kundi I sasa ni Gabon pointi saba, Mauritani nne na Sudan tatu kama DRC kueleka mechi za katikati ya wiki ijayo.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE ATOKEA BENCHI DRC YASHINDA 3-1 KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top