• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  TAIFA STARS YAICHAPA UGANDA 1-0 MISRI BAO LA MSUVA  TANZANIA imeweka hai matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Uganda bao la Simon Msuva kwenye mchezo wa Kundi F leo Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri.
  Msuva anayechezea klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia amefunga bao hilo dakika ya 68 akimalizia krosi ya beki wa Yanga, Dickson Job na kumpa mwanzo mzuri kocha Mualgeria, Adel Amrouche Taifa Stars.
  Ushindi huo unaifanya Taifa Stars fikishe pointi nne na kusogea nafasi ya pili nyuma ya Algeria yenye pointi tisa, wakati Uganda inayobaki na pointi yake moja inashika mkia nyuma ya Niger yenye pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi tatu. 
  Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAICHAPA UGANDA 1-0 MISRI BAO LA MSUVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top