• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2023

  CHAMA AENDA KUISAIDIA NA CHIPOLOPOLO VITA YA AFCON


  KIUNGO wa Simba SC, Clatous Chama akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa safari ya kwao, Zambia kwenda kujiunga na timu yake ya taifa, Chipolopolo kwa ajili ya mchezo wa Kundi H kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Lesotho Alhamisi Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  Chama anakwenda kujiunga na Chipolopolo baada ya kuisaidia Simba kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam akifunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Horoya ya Guinea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA AENDA KUISAIDIA NA CHIPOLOPOLO VITA YA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top