• HABARI MPYA

  Sunday, March 26, 2023

  RAIS AWANUNULIA TIKETI MASHABIKI 7000 WAKAISHANGILIE TAIFA STARS DHIDI YA UGANDA  KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu leo amekabidhi tiketi Elfu 20 Kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya Mashabiki kuingia uwanjani kuishangilia Taifa Stars Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
  Akizungumza  na Waandishi wa Habari, wakati wa kukabidhi tiketi hizo, leo Machi 26, 2023 jijini Dar es  Salaam, Katibu Mkuu Yakubu, amesema tiketi hizo zinajumuisha tiketi 7000 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tiketi 2000 za Waziri Mkuu Mhe. Kassim  Majaliwa na Tiketi 11, 000 za Wizara yake pamoja na wadau wa wizara hiyo waliounga mkono zoezi hilo.  "Tunamshukuru Rais kwa mchango wake katika Sekta ya Michezo, baada ya ushindi wa juzi ameongeza hamasa kwa kununua kila goli kwa shilingi Milioni 10, hili ni jambo kubwa, nawaomba Watanzania tujitokeze uwanjani tuishangilie timu yetu, wapate nguvu za kupata ushindi, amesema Katibu Mkuu Yakubu.
  Taifa stars itacheza mchezo wa marudiano na Uganda The Cranes Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo wa awali waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 mchezo uliochezwa katika mji wa Ismailia nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS AWANUNULIA TIKETI MASHABIKI 7000 WAKAISHANGILIE TAIFA STARS DHIDI YA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top