• HABARI MPYA

  Sunday, March 26, 2023

  MOROCCO YAICHAPA BRAZIL 2-1 MECHI YA KIRAFIKI


  TIMU ya Taifa ya 
  Morocco jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brazil 
  kwenye mchezo wa kirafiki mjini Tangiers.
  Sofiane Boufal alianza kuifungia Morocco dakika ya 29, kabla ya Nahodha wa Brazil, Casemiro kusawazsha dakika ya 67 na Abdelhamid Sabiriakawafumgia wana Nusu Fainali ya Kombe la Dunia bao la ushindi dakika ya 79 huo ukiwa ushindi wa kwanza daima dhidi ya Brazil.
  Baada ya mchezo huo, kocha wa muda wa Brazil, Ramon Menezes alikacha mkutano na Waandishi wa Habari, wakati Kocha wa Morocco, Walid Regragui alifurahia ushindi huo unaofuatia mafanikio yake katika Kombe la Dunia Desemba mwaka jana nchini Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO YAICHAPA BRAZIL 2-1 MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top