• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2023

  AZAM FC KUCHEZA NA GOR MAHIA JUMAPILI NAIROBI


  KLABU ya Azam FC itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na baada ya hapo itasafiri kwenda Kenya kwa ajili ya mchezo na wenyeji, Gor Mahia Jumapili.
  Taarifa ya Azam FC imesema kwamba kikosi kitaondoka Dar es Salaam Ijumaa kwenda kwneye mechi dhidi ya Gor Mahia itakayochezwa Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi kuanzia Saa 9:00 Alasiri.
  Kuhusu mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar, itafanyika Uwanja wa Azam Complex Saa 1.00 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA NA GOR MAHIA JUMAPILI NAIROBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top