• HABARI MPYA

  Tuesday, March 28, 2023

  YANGA YAMFUKUZA KOCHA WA TIMU YA WANAWAKE


  UONGOZI wa klabu ya Yanga umeachana na Kocha Mkuu wa timu ya wanawake, Thobias Nkoma na kwa sasa kikosi kitakuwa chini ya aliyekuwa Msaidizi wake, Freddy Mbuna.
  Hatua inachukuliwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara licha ya kile ambacho uongozi unaamini uwekezaji mkubwa walioufanya kikosini.
  Kwa sasa Yanga Princess inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Wanawake kwa pointi zake 22, nyuma ya watani, Simba Queens 27, JKT Queens 28 na Fountain Gate Princess 29 baada ya wote kucheza mechi 12.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMFUKUZA KOCHA WA TIMU YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top