• HABARI MPYA

  Sunday, March 19, 2023

  WAZIRI WA MICHEZO ALIVYOWAKABIDHI YANGA MAMILIONI YA RAIS SAMIA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Pindu Chana akimkabidhi Nahodha wa Yanga SC, Bakari Nondo Mwamnyeto Sh. Milioni 10 ambazo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.  Rais Samia ametoa zawadi ya Sh. Milioni 5 kwa kila bao walilofunga Yanga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya US Monastirienne ya Tunisia leo kwenye mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO ALIVYOWAKABIDHI YANGA MAMILIONI YA RAIS SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top