• HABARI MPYA

  Tuesday, March 28, 2023

  SENEGAL YAICHAPA MSUMBIJI 1-0 MAPUTO


  MABINGWA watetezi, Senegal wamejihakikishia kufuzu Fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Msumbiji katika mchezo wa Kundi L leo Uwanja wa Taifa wa Zimpeto Jijini Maputo.
  Bao pekee la Simba wa Teranga leo limefungwa na mshambuliaji wa Salernitana ya Italia, Boulaye Dia dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri ya Nahodha, Sadio Mane wa Bayern Munich.
  Nyota wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pape Ousmane Sakho ameendelea kuwa mchezaji akiba kwa muda wote katika mchezo wa pili mfululizo leo aitwr mara ya kwanza kwenye kikksi cha Aliou Cissé.
  Ushindi wa leo unaifanya Senegal ifikishe pointi 12, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye Kundi hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL YAICHAPA MSUMBIJI 1-0 MAPUTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top