• HABARI MPYA

  Monday, March 27, 2023

  MASHABIKI KUINGIA BURE MECHI YA STARS ENEO LOTE LA MZUNGUKO

  ENEO la mzunguko mashabiki wataingia bure kesho katika mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kwamba hiyo inatokana na wadau mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwanunulia tiketi mashabiki. 
  Taifa Stars itaingia dimbani katika mchezo utakaoanza Saa 2:00 usiku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda Ijumaa Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri, bao pekee la Simon Msuva.


  Kwa sasa Taifa Stars inashika nafasi ya pili Kundi F kwa pointi zake nne, nyuma ya Algeria yenye pointi tisa na mbele ya Niger yenye pointi mbili na Uganda pointi moja baada ya mechi tatu za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHABIKI KUINGIA BURE MECHI YA STARS ENEO LOTE LA MZUNGUKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top