• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  RONALDO APIGA MBILI URENO YASHINDA 4-0 KUFUZU EURO 2024

  NAHODHA Cristiano Ronaldo jana alifunga mabao mawili timu yake ya taifa, Ureno ikiibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Liechtenstein katika mchezo wa Kundi J kufuzu Euro 2024 Uwanja wa José Alvalade Jijini Lisbon, Ureno.
  Akicheza mechi ya kwanza tangu Kombe la Dunia la Qatar Desemba, Ronaldo alifunga bao la tatu kwa penalti dakika ya 51 na lingine kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 63 katika staili yake maarufu.
  Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Joao Cancelo dakika ya nane na Bernardo Silva dakika ya 45 kikosi cha Roberto Martinez kikianza vyema mbio za Euro ya mwakani Ujerumani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA MBILI URENO YASHINDA 4-0 KUFUZU EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top