• HABARI MPYA

  Thursday, March 30, 2023

  WAPINZANI WA SIMBA NA YANGA ROBO FAINALI AFRIKA HADHARANI JUMATANO


  DROO ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika itafanyika Jumatano ijayo, Aprili 5 makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jijini Cairo, Misri kuanzia Saa 3:30 usiku.
  Na hiyo itafuatia mechi za mwisho za Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa wikiendi hii.
  Timu ambazo tayari zimefuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni; 
  CR Belouizdad (Algeria), Esperance Tunis (Tunisia), JS Kabylie (Algeria), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Raja Casablanca (Morocco), Simba SC (Tanzania), Wydad AC (Morocco), Al Ahly (Misri) au Al Hilal (Sudan) 
  Na kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni; Rivers United (Nigeria), ASFAR Club (Morocco), US Monastir (Tunisia), Asec Mimosas (Ivory Coast), Marumo Gallants (Afrika Kusini), Yanga SC (Tanzania), Pyramids FC (Misri) au Future FC (Misri), Al Akhdar SC (Libya) or FC Saint Éloi Lupopo (DRC) au USM Alger (Algeria).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAPINZANI WA SIMBA NA YANGA ROBO FAINALI AFRIKA HADHARANI JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top