• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  CHAMA NA MUSONDA WASHUHUDIA ZAMBIA IKISHINDA 3-1  NYOTA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Clatous Chama wa Simba na Kennedy Musonda wa Yanga wote walikuwa nje jana Zambia ikishinda 3-1 dhidi ya Lesotho Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola katika mchezo wa Kundi H kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast.
  Mabao ya Chipolopolo yalifungwa na mshambuliaji wa Rangers ya Scotland, Fashion Sakala dakika ya 37 na kiungo wa Lecce ya Italia, Lameck Banda dakika ya 53 na 57, wakati la Lesotho lilifungwa na kiungo wa Mbabane Highlanders ya Eswatini, dakika ya 33 Tshwarelo Bereng.
  Kwa ushindi huo, Zambia inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Muisrael Avram Grant panda kileleni kwa Kundi H ikifikisha pointi sita katika mchezo wa tatu, ingawa Ivory Coast wanaweza kurejea juu wakiifunga Comoro leo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA NA MUSONDA WASHUHUDIA ZAMBIA IKISHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top