• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2023

  ROBO FAINALI ASFC; SIMBA UHURU APRILI 7, YANGA CHAMAZI APRILI 8


  ROBO Fainali za Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitaanza Aprili 2 kwa mchezo kati ya Singida Big Stars na Mbeya City Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Robo Fainali ya pili itafuatia Aprili 3 kwa mchezo kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Robo Fainali ya tatu ni Aprili 7 baina ya Simba SC na Ihefu Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watakamilisha ngwe hiyo kwa kumenyanana na Geita Gold Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Aprili 8.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBO FAINALI ASFC; SIMBA UHURU APRILI 7, YANGA CHAMAZI APRILI 8 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top