• HABARI MPYA

  Tuesday, March 28, 2023

  TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR

  WENYEJI, Tanzania wamechapwa bao 1-0 na Uganda katika mchezo wa Kundi F Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars leo limefungwa na winga wa KCCA ya nyumbani, Kampala, Rogers Mato Kassim dakika ya 90 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Farouk Miya wa Rizespor ya Uturuki.
  Matokeo hayo yanazidi kuliweka pagumu Kundi F kuelekea mechi mbili za mwisho, kwani sasa ukiondoa Algeria ambayo imekwishafuzu kwa pointi zake 12, Tanzania na Uganda zenye pointi nne kila na Niger yenye pointi mbili moja wapo unaweza kufuzu pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top