• HABARI MPYA

  Saturday, March 25, 2023

  MAPRO WA UARABUNI WAKITETA STARS IKIREJEA DAR


  WACHEZAJI wa Tanzania wanaocheza Uarabuni, Simon Msuva wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia (kulia) na Said Khamis Said wa Al Baniyas ya Falme za Kiarabu (UAE) wakiwa safarini kurejea nyumbani, Dar es Salaam kutoka Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Uganda kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Jumanne.


  Nahodha Mbwana Samatta (kulia) wa KRC Genk ya Ubelgiji safarini pia. Taifa Stars watakuwa wenyeji wa The Cranes Jumanne katika mchezo wa Kundi F kufuzu AFCON baada ya jana Tanzania kushinda 1-0 dhidi ya Uganda mjini Ismailia nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAPRO WA UARABUNI WAKITETA STARS IKIREJEA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top