• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  MBRAZIL WA SINGIDA BIG STARS HADI MSIMU UJAO TENA


  NYOTA wa Singida Big Stars, Dario Frederico amemaliza ruhusa ya mwezi mmoja ya matibabu nchini kwao, Brazil na ripoti ya daktari inaonesha amepona kwa zaidi ya asilimia 90.
  Klabu kupitia kwa ushauri wa kitaalamu wa daktari imemuongezea muda Dario Jr ili aweze kuwa timamu kwa asilimia 100.
  Singida Big Stars imesema kwamba kutokana na maamuzi hayo, mchezaji huyo ataungana na kikosi rasmi wakati wa maandalizi msimu ujao.
  Wadau na mashabiki wa Singida Big Stars watarajie kumuona Dario akiwa kwenye kiwango bora zaidi atakapoungana na timu kwenye kambi hiyo nchini Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBRAZIL WA SINGIDA BIG STARS HADI MSIMU UJAO TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top