• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2023

  MAYELE HUYOO AENDA KUIPIGANIA DRC KOMBE LA AFRIKA


  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa safari ya kwenda kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga na timu yake ya taifa kwa ajili ya mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Mauritania Ijumaa Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi.

  Mayele ameongozana na beki wa Simba, Henock Inonga Baka ‘Varane’ ambaye wameitwa naye timu ya taifa. Na hapa walikutana na wachezaji walioitwa timu ya taifa ya Zambia, kiungo Clatous Chama wa Simba na mshambuliaji Kennedy Musonda wa Yanga.
  Mayele na Musonda kila mmoja alifunga bao moja Yanga ikishinda 2-0 dhidi ya US Monastirienne katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam
  na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE HUYOO AENDA KUIPIGANIA DRC KOMBE LA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top