• HABARI MPYA

    Saturday, March 25, 2023

    SAKHO AMSHUHUDIA MANE AKIIONGOZA SENEGAL KUICHAPA MSUMBIJI 5-1


    MSHAMBULIAJI wa Simba, Pape Ousmane Sakho jana alikuwa benchi muda wote Senegal ikiichapa Msumbiji 5-1 Uwanja wa Me Abdoulaye Wade, Diamniadio katika mchezo wa Kundi L Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.
    Mabao ya Simba wa Teranga yalifungwa na beki wa Real Betis, Youssouf Sabaly dakika ya tisa, mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane dakika ya 15 na kiungo wa Sheffield United Iliman Ndiaye dakika ya 32.
    Mengine yalifungwa mshambuliaji wa Salernitana ya Italia, Boulaye Dia dakika ya 39 na mshambuliaji wa Strasbourg ya Ufaransa, Mouhamadou Habibou Diallo, wakati la Msumbiji lilifungwa na kiungo wa Sporting Covilhã ya Ureno, Gildo Vilanculos dakika ya 48.
    Simba wa Teranga wanafikisha pointi  tisa na kuendelea kuongoza Kundi L mbele ya Msumbiji pointi nne, Rwanda mbili na Benin moja.
    Sakho aliyeitwa mara ya kwanza kabisa timu ya taifa ya Senegal ndiye mchezaji pekee anayecheza klabu ya Afrika kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi za tatu na za nne kufuzu AFCON 2023.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAKHO AMSHUHUDIA MANE AKIIONGOZA SENEGAL KUICHAPA MSUMBIJI 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top