• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UTEKELEZAJI WIZARA YA UTAMADUNI


  KAMATI ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na Bajeti iliyotengewa kwa mwaka wa fedha 2022/23.
  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo ametoa pongezi hizo leo Machi 23, 2023 jijini Dodoma, wakati Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya Utekelezaji wa Wizara kwa mwaka wa Fedha 2022/23, ambapo amesema Wizara imendeleea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kusaidia wadau kunufaika na kazi zao pamoja na kutatua migogoro inayoibuka miongoni mwa wadau wa Sekta zake.
  "Wizara hii ndiyo inayotoa furaha kwa Watanzania, sisi kama Wabunge tunataka kuona utulivu kwenye Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, tuendelee kuwatia moyo vijana wetu wafanye kazi ili tuwe tunasikia mambo mazuri"  Amesisitiza Mhe. Mkumbo.
  Awali akiwasilisha taarifa ya Wizara, Waziri Balozi Dk. Pindi Chana amesema kwa mwaka wa Fedha 2022/23 wizara imefanikiwa kuanzisha upya mchakato wa Vazi la Taifa, kuendelea kubidhaisha kiswahili pamoja na Kuratibu na kuandaa Tamasha la Utamaduni na Siku ya Kiswahili.
  Waziri Pindi Chana ameeleza kuwa, Wizara imefanikiwa kuratibu ushiriki wa Timu za Taifa katika mashindano ya Kombe la Dunia ikiwemo Serengeti Girls na Tembo Warriors ambazo zote zilifika hatua ya Robo fainali, huku akiongeza kuwa tayari Serikali inamlipa  Kocha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars)
  Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo wamechambua taarifa hiyo kwa nyakati fofauti ambapo wamesisitiza Wizara kuendelea kusimamia sekta hizo ambazo zimeajiri vijana wengi zaidi.
  Kikao hicho pia kimehudhuriwa na baadhi ya  Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais, Wallace Karia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UTEKELEZAJI WIZARA YA UTAMADUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top