• HABARI MPYA

  Sunday, March 26, 2023

  AMROUCHE AWAREJESHA KIKOSINI TAIFA STARS KAPOMBE NA TSHABALALA


  KOCHA Mualgeria wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche amewaongeza kikosini mabeki wa pembeni wa Simba SC, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuelekea mchezo na Uganda Jumanne.
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa The Cranes keshokutwa katika mchezo wa Kundi F kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ikihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.
  Kapombe na Tshabalala wote hawakuwemo kwenye kikosi kilichoshinda 1-0 dhidi ya Uganda juzi Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri, bao pekee la Simon Msuva kutokana na kutojumuishwa kwenye kikosi cha kwanza kwa Amrouche baada ya kuanza kazi Tanzania.
  Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Shilingi Milioni 10 kwa kila bao litakalofungwa kwenye mechi ya keshokutwa.
  Kwa sasa Taifa Stars inashika nafasi ya pili Kundi F kwa pointi nne, nyuma ya Algeria yenye pointi tisa na mbele ya Niger yenyebpointi mbili na Uganda pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMROUCHE AWAREJESHA KIKOSINI TAIFA STARS KAPOMBE NA TSHABALALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top