• HABARI MPYA

  Monday, March 27, 2023

  RONALDO AFUNGA MBILI TENA URENO YASHINDA 6-0

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo jana amefunga tena manao mawili kwa mara ya pili mfululizo akiiwezesha Ureno kuichapa Luxembourg 6-0 katika mchezo wa Kundi J kufuzu Euro 2024 Uwanja wa Luxembourg mjini Lëtzebuerg (Luxembourg. 
  Ronaldo (38) alifunga dakika ya tisa na 31, wakati mabao mengine yalifungwa na João Félix dakika ya 15, Bernardo Silva dakika ya 18, Otávio dakika ya 77 na Rafael Leão dakika ya 88.
  Ureno inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi J kwenye mbio za Euro 2024 nchini Ujerumani, ikifuatiwa na Slovakia pointi nne, Bosnia-Herzegovina pointi tatu sawa na Iceland, Luxembourg pointi moja, wakati Liechtenstein haina kitu baada ya mechi mbili za awali.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA MBILI TENA URENO YASHINDA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top