• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  BALOZI NCHIMBI AKABIDHIWA JEZI NAMBA 29 TAIFA STARS

   


  KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  Kidao Wilfred akimkabidhi jezi namba 29 ya Timu ya Taifa Balozi wa Tanzania Nchini Misri, Dk. Emmanuel Nchimbi kuelekea mchezo dhidi ya  Uganda leo Saa 11:00 jioni kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023.
  Mchezo huo wa Kundi F utafanyika Uwanja wa Suez Canal Jijini Ismailia, kabla ya timu hizo kurudiana Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Awali ya hapo, Kidau alimkabidhi Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma jezi namba 25 ya Taifa Stars hapo hapo Ismailia jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOZI NCHIMBI AKABIDHIWA JEZI NAMBA 29 TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top