• HABARI MPYA

  Friday, March 24, 2023

  RAIS SAMIA KUZAWADIA MILIONI 10 KILA BAO TAIFA STARS


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan aipongeza timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda leo nchini Misri.
  Aidha, kuelekea mchezo wa marudiano Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Rais Samia ameahidi kutoa Shilingi Milioni 10 kwa kila bao litakalofungwa.
  Taifa Stars imeweka hai matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Uganda kwenye mchezo wa Kundi F leo Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri.
  Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Simon Msuva anayechezea klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia 
  dakika ya 68 akimalizia krosi ya beki wa Yanga, Dickson Job na kumpa mwanzo mzuri kocha Mualgeria, Adel Amrouche Taifa Stars.
  Ushindi huo unaifanya Taifa Stars fikishe pointi nne na kusogea nafasi ya pili nyuma ya Algeria yenye pointi tisa, wakati Uganda inayobaki na pointi yake moja inashika mkia nyuma ya Niger yenye pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi tatu. 
  Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA KUZAWADIA MILIONI 10 KILA BAO TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top