• HABARI MPYA

  Sunday, March 26, 2023

  CHAMA NA MUSONDA WATOKEA BENCHI ZAMBIA YASHINDA 2-0


  NYOTA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Clatous Chama na Kennedy Musonda wametokea benchi kuichezea Zambia dakika za mwishoni ikishinda 2-0 dhidi ya Lesotho kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Katika mchezo huo wa Kundi H uliofanyika Uwanja wa Volkswagen Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini - mabao ya Chipolopolo yote yamefungwa na mshambuliaji wa Leicester City, Patson Daka dakika ya 14 na 69.
  Kiungo wa Simba, alianza kuingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Kings Kangwa wa Red Star Belgrade ya Serbia, akafuatia mshambuliaji wa Yanga, Musonda kuingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mfungaji wa mabao, Patson Daka.
  Ushindi wa leo unaifanya Zambia ifikishe pointi tisa katika mchezo wa nne na kupanda kileleni ikiizidi Ivory Coast pointi mbili ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA NA MUSONDA WATOKEA BENCHI ZAMBIA YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top