• HABARI MPYA

  Friday, March 31, 2023

  BILIONEA GHALIB MAZOEZINI YANGA LUBUMBASHI LEO


  BILIONEA Gharib Said Mohamed (katikati) akiwa na Rais wa Yanga SC, Hersi Ally Said na Makamu wake, Arafat Hajji (kulia) wakijadiliana wakati wa mazoezi ya timu leo Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  Tayari mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda (kishoto) aliyekuwa na timu yake ya Taifa, Chipolopolo amekwishajiunga na Yanga kuelekea mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, TP Mazembe Jumapili.  Kiungo Mkongo Yanick Bangala anaonekana yuko fiti kabisa kuelekea mchezo huo dhidi ya timu ya nyumbani kwao, DRC.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BILIONEA GHALIB MAZOEZINI YANGA LUBUMBASHI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top