• HABARI MPYA

  Friday, October 08, 2021

  UFARANSA YAICHAPA UBELGIJI 3-2 ITALIA


  UFARANSA imefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ubelgiji usiku wa jana Uwanja wa Allianz Jijini Torino nchini Italia.
  Ubelgiji walitangulia kwa mabao ya Yannick Carrasco dakika ya 37 na Romelu Lukaku dakika ya 40, kabla ya Ufaransa kutoka nyuma kwa mabao ya Karim Benzema dakika ya 62, Kylian Mbappe kwa penalti dakika ya 69 na Theo Hernandez dakika ya 90.
  Sasa Ufaransa itakutana na Hispania katika fainali tamu ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya Jumapili Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, wakati Ubelgiji itawania nafasi ya tatu dhidi ya wenyeji, Italia keshokutwa pia Uwanja wa Allianz, Turin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YAICHAPA UBELGIJI 3-2 ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top