• HABARI MPYA

  Friday, October 08, 2021

  MAUYA KUZIBA PENGO LA MUZAMIL STARS


  KIUNGO wa Yanga SC, Zawadi Mauya ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano Kundi J kufuzu Kombe la Dunia mwakani Qatar.
  Kocha Mdenmark, Kim Poulsen amelazimika kumuita Mauya kufuatia kiungo wa Simba SC, Muzamil Yassin kuonyeshwa kadi ya pili ya njano jana katika mchezo dhidi ya Benin.
  Taifa Stars imeondoka mapema leo asubuhi kwenda Cotonou kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Benin Jumapili kufuatia jana kuchapwa 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Taifa Stars inahitaji kulipa kisasi kwa kushinda ugenini ili kufufua matumaini ya kwenda hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Qatar 2022.
  Kwa sasa Taifa Stars ni ya tatu Kundi J kwa pointi zake nne, mbele ya Madagascar ambayo haina pointi na nyuma ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pointi tano na Benin pointi saba baada ya mechi tatu za mwanzo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAUYA KUZIBA PENGO LA MUZAMIL STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top