• HABARI MPYA

  Sunday, October 24, 2021

  NDAYIRAGIJE KOCHA WA KWANZA KUFUKUZWA LIGI KUU


  KLABU ya Geita Gold imekuwa timu ya kwanza kufukuza kocha msimu huu baada ya raundi nne za bila ushindi, ikifungwa mechi mbili zote ugenini na droo mbili zote nyumbani.
  Baada ya kufungwa mechi ya kwanza 2-0 na Namungo FC mjini Lindi na 1-0 na Yanga Jijini Dar es Salaam, ilitoa sare za 1-1 mfululizo nyumbani na Mtibwa Sugar na Mbeya City.
  Baada ya sare ya jana Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita, mashabiki walimghasi kocha Mrundi, Ettiene Ndayiragije kabla ya saa chache baadaye uongozi kutangaza kuachana naye.
  Mrundi huyo aliyewahi kufundisha Mbao FC ya Mwanza, KMC na Azam FC za Dar es Salaam na timu ya taifa, Taifa Stars alianza kazi Geita baada ya kupanda Daraja chini ya kocha Mzalendo, Freddy Felix Minziro.
  Taarifa ya kufukuzwa kwa kocha huyo imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Ndayiragije kushindwa kufikia malengo waliyokubaliana na sasa timu hiyo itakuwa chini ya Minziro.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDAYIRAGIJE KOCHA WA KWANZA KUFUKUZWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top