• HABARI MPYA

  Friday, October 15, 2021

  BIASHARA UNITED YAICHAPA AL AHLI 2-0


  TIMU ya Biashara United ya Mara imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa kwanza Raundi ya Pili, mabao ya Biashara United inayofundishwa na kocha Mkenya, Patrick Odhiambo anayesaidiwa na mzawa, Marwa Chamberi yamefungwa na Deogratius Judika Mafie dakika ya 40 na Atupele Green Jackson dakika ya 61.
  Mchezo wa marudiano utafanyika Jumamosi ijayo, Oktoba 23 Uwanja wa Martyrs of February Jijini Benghazi nchini Libya na mshindi wa jumla atamenyana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAICHAPA AL AHLI 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top