• HABARI MPYA

  Saturday, October 30, 2021

  LIVERPOOL YADUWAZWA NYUMBANI NA BRIGHTON


  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 2-2 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.
  Liverpool ilitangulia kwa mabao ya Jordan Henderson dakika ya nne na Sadio Mane dakika ya 24, kabla ya Brighton kuzinduka kwa mabao ya Enock Mwepu dakika ya 41 na Leandro Trossard dakika ya 65.
  Kwa sare hiyo ya nyumbani, kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 22, kikizidiwa pointi tatu na Chelsea inayoongoza baada ya wote kucheza mechi 10.
  Brighton yenyewe baada ya sare ya leo inafikisha pointi 16 kufuatia kucheza mechi 10 pia kikisogea nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YADUWAZWA NYUMBANI NA BRIGHTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top