• HABARI MPYA

  Friday, October 29, 2021

  KAGERA SUGAR YAICHAPA KMC 1-0 UHURU


  BAO la Meshack Abraham dakika ya 16 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Kagera Sugar ifikishe pointi nane baada ya mechi tano na kupanda nafasi ya tatu nyuma ya Polisi Tanzania na Yanga zenye pointi tisa kila moja, wakati KMC inabaki na pointi mbili baada ya mechi tano pia.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Mbeya Kwanza imelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kiungo mkongwe Ramadhani Suleiman Chombo ‘Redondo’ alianza kuifungia Biashara United dakika ya 13, kabla ya mshambuliaji Hamisi Kanduru kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 81.
  Wakati Mbeya Kwanza inafikisha pointi sita, Biashara United imetimiza pointi tano katika mechi nne wote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA KMC 1-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top