• HABARI MPYA

  Wednesday, October 20, 2021

  LIVERPOOL YAICHAPA ATLETICO 3-2 HISPANIA


  TIMU ya Liverpool jana imewachapa wenyeji, Atletico Madrid. mabao 3-2 katika mchezo wa Kundi Uwanja wa Wanda Metropolitano Jijini Madrid.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah dakika ya nane akimalizia pasi ya Andrew Robertson na dakika ya 78 kwa penalti baada ya Diogo Jota kuchezewa rafu na Naby Keita dakika ya 13.
  Kwa upande wao, Atletico Madrid mabao yao yalifungwa na Antoine Griezmann yote dakika ya 20 na 34 kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 52 kwa kumchezea rafu Roberto Firmino.
  Liverpool inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi B kwa pointi tano zaidi ya Atletico Madrid na Porto zenye pointi nne kila moja, huku AC Milán ikiwa inashika mkia haina pointi baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA ATLETICO 3-2 HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top