• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  CHELSEA YASHINDA 4-0 LUKAKU NA TIMO WAUMIA


  WENYEJI, Chelsea wameitandika Malmo mabao 4-0 usiku wa Jumatano katika mchezo wa Kundi  H Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya mabingwa hao watetezi, The Blues yamefungwa na Andreas Christensen dakika ya tisa, Jorginho mawili yote kwa penalti dakika ya 21 na 57 na Kai Havertz dakika ya 48.
  Lakini Chelsea ilipata pigo baada ya washambuliaji wake wawili pacha kushindwa kumalizia mechi kufuatia kuumia, Romelu Lukaku aliyempisha Kai Havertz dakika ya 23 na Timo Werner aliyempisha Callum Hudson-Odoi dakika ya 44.
  Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi sita, ingawa inabaki nafasi ya pili ilizidiwa pointi tatu na Juventus inayoongoza, wakati Malmo inaendelea kushika mkia ikiwa haina pointi na nafasi ya tatu ipo Zenit yenye pointi tatu baada ya mechi tatu za mwanzo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YASHINDA 4-0 LUKAKU NA TIMO WAUMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top