• HABARI MPYA

  Wednesday, October 06, 2021

  MAKOCHA WAPYA WA VIJANA AZAM FC


  KLABU ya Azam FC imetambulisha makocha wawili wa timu zake za vijana, Mohamed Badru, U-17 na Mussa Rashid U-20.
  Badru amewahi kufundisha klabu za Mtibwa Sugar, Gwambina na Malindi ya kwao, Zanzibar na Rashid amefundisha African Sports ya Tanga na kila mmoja amesaini mkataba wa miaka miwili.
  Wawili hao wanakwenda kuchukua majukumu yaliyokuwa yanafanywa na Mrundi, Vivier Bahati, ambaye amepandishwa kwenda timu kubwa ya Azam FC, akiwa Kocha Msaidizi wa George Lwandamina.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKOCHA WAPYA WA VIJANA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top