• HABARI MPYA

  Friday, October 15, 2021

  BRAZIL YAICHAPA URUGUAY 4-1 KOMBE LA DUNIA


  WENYEJI, Brazil wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Uruguay katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia kwa Amerika Kusini usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Arena da Amazônia Jijini Manaus, Amazonas.
  Mabao ya Brazil yamefungwa na Neymar dakika ya 10, Raphinha mawili dakika ya 18 na 58 na Gabriel Barbosa dakika ya 83, wakati la Uruguay limefungwa na Luis Suárez dakika ya 77.
  Kwa ushindi huo, Brazil inafikisha pointi 31 na kuendelea kuongoza mbio za kuwania tiketi ya Qatar mwakani kwa Amerika Kusini kwa pointi sita zaidi ya Argentina inayofuatia baada ya mechi 11 wote.
  Na hiyo ni baada ya Argentina kuichapa Peru 1-0 bao pekee la Lautaro Martínez dakika ya 43 Uwanja wa Monumental Antonio Vespucio Liberti, Capital Federal, Ciudad de Buenos Aires.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YAICHAPA URUGUAY 4-1 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top