• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  HATIMAYE BARCELONA YASHINDA MECHI ULAYA


  HATIMAYE Barcelona imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Dynamo Kiev 1-0, bao pekee la mlinzi Gerard Pique katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa Camp Nou.
  Kwa pointi hizo tatu za kwanza baada ya mechi tatu Barcelona inayofundishwa na kocha Ronald Koeman inapanda nafasi ya tatu, mbele ya Dynamo Kiev yenye pointi moja na nyuma ya Benfica yenye pointi nne na vinara, Bayern Munich wenye pointi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMAYE BARCELONA YASHINDA MECHI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top