• HABARI MPYA

  Sunday, October 24, 2021

  DODOMA JIJI YAICHAPA PRISONS 2-1 DODOMA


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 37 kwa penalti na Emmanuel Martin dakika ya 59, wakati la Prisons limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya tatu.
  Dodoma Jiji wanafikisha pointi saba baada ya mechi nne na kusogea nafasi ya tatu wakizidiwa pointi mbili na Yanga na Polisi Tanzania ambazo zimecheza mechi tatu kila moja.
  Tanzania Prisons inabaki na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA PRISONS 2-1 DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top