• HABARI MPYA

  Saturday, October 23, 2021

  SAMATTA AWAADHIBU FENERBAHCE PALE PALE ISTANBUL

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta juzi aliifunga klabu yake, Fenerbahce ya Uturuki akicheza kwa mkopo Royal Antwerp ya Ubelgiji, lakini hakushangilia.
  Katika mchezo wa ugenini wa Kundi D UEFA Europa League uliofanyika Uwanja wa Ulker Fenerbahçe Şükrü Saracoğlu Spor Kompleksi Jijini İstanbul nchini Uturuki, Samatta aliifungia bao la kwanza Antwerp dakika ya pili timu hizo zikitoka sare ya 2-2.
  Lakini Fenerbahce ikazinduka kwa mabao ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ecuador, Enner Valencia dakika ya 20 na la penalti dakika ya 45, kabla ya kiungo Mbelgiji Pieter Gerkens kuisawazishia Royal Antwerp dakika ya 62.


  Kwa sare hiyo, Royal Antwerp wanaokota pointi ya kwanza na Fenerbahce pointi ya pili wakiendelea kuwa nyuma ya Eintracht Frankfurt yenye pointi saba na Olympiakos pointi sita baada ya kila timu kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AWAADHIBU FENERBAHCE PALE PALE ISTANBUL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top