• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  SANE APIGA MBILI, BAYERN MUNICH YASHINDA 4-0


  WENYEJI, Benfica wamechapwa mabao 4-0 na Bayern Munich katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Luz Jijini Lisbon, Ureno.
  Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sane mawili dakika ya 70 na 84, Éverton aliyejifunga dakika ya 80 na Robert Lewandowski dakika ya 82.
  Bayern Munich inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi E, ikifuatiwa na Benfica yenye pointi nne, Barcelona pointi tatu na
  Dynamo Kiev yenye pointi moja baada ya mechi tatu za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANE APIGA MBILI, BAYERN MUNICH YASHINDA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top