• HABARI MPYA

  Wednesday, October 13, 2021

  RAIS SAMIA AWAAHIDI JAMBO TWIGA, TANZANITE


  RAIS WA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan jana alizungumza kwa simu na wachezaji wa taifa ya wakubwa ya wanawake, Twiga Stars na ya wasichana chini ya umri miaka 20, Tanzanite na kuahidi kuwafanyia jambo akirejea Dar es Salaam.
  Mama Samia alizungumza na wachezaji hao jana kupitia simu ya Katibu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa hafla maalum ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Serikali kuwapongeza wachezaji hao kwa mafanikio yao.  
  Wakati Twiga Stars ilitwaa ubingwa wa COSAFA Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, wadogo zao Tanzanite waliitoa Eritrea katika mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia la U20 mwakani Costa Rica.
  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas ametoa ahadi kwa niaba ya Serikali ya Sh. Milioni 20 kwa Twiga Stars kutwaa ubingwa wa COSAFA na Sh. Milioni 10 kwa Tanzanite kwa kuingia raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA AWAAHIDI JAMBO TWIGA, TANZANITE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top