• HABARI MPYA

  Sunday, October 24, 2021

  AZAM FC YATUPWA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


  TIMU ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Pyramids bao pekee la Ally Gabri Mossad dakika ya 29 usiku wa jana Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo, Misri.
  Hiyo inafuatia Azam FC kulazimishwa sare ya 0-0 na timu hiyo ya Misi katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
  Sasa Pyramids itamenyana na moja ya timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATUPWA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top