• HABARI MPYA

  Wednesday, October 27, 2021

  SIMBA SC YAPOZA MACHUNGU YA GALAXY


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamefuta machozi ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani wenyeji hao walilazimika kusubiri hadi dakika ya 89 kupata bao hilo pekee tena kwa mkwaju wa penalti wa kiungo Mzambia, Rally Bwalya.
  Simba SC inafikisha pointi saba baada ya mechi tatu, kufuatia kutoa sare mechi ya kwanza na Biashara United mjini Musoma mkaoni Mara kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Dodom Jiji FC mjini Dodoma.
  Polisi Tanzania ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya mwanzo mzuri wakishinda mechi tatu mfululizo leo wamepoteza mechi ya kwanza.
  Ikumbukwe Simba ilifungwa 3-1 na Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumapili katika mchezo wa kuwania kuingia Hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na kutolewa kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza Gaborone.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAPOZA MACHUNGU YA GALAXY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top