• HABARI MPYA

  Saturday, October 23, 2021

  CHELSEA YAITANDIKA NORWICH CITY 7-0 DARAJANI

  TIMU ya Chelsea imewatandika vibonde, Norwich City mabao 7-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya The Blues yamefungwa na Mason Mount matatu dakika za nane, 85 kwa penalti na 90 na ushei, Callum Hudson-Odoi dakika ya 18, Reece James dakika ya 42, Ben Chilwell dakika ya 57 na Max Aarons aliyejifunga dakika ya 62.
  Beki Ben Gibson alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Reece James.


  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
  Norwich City inabaki na pointi mbili baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuzibeba timu nyingine 19 katika Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAITANDIKA NORWICH CITY 7-0 DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top