• HABARI MPYA

  Sunday, October 10, 2021

  TYSON FURY AMTWANGA TENA WILDER KWA KO

  BONDIA Muingereza, Tyson Fury amempiga Mmarekani Deontay Wilder kwa Knockout (KO) raundi ya 11 kwenye pambano la raundi 12 asubuhi ya leo ukumbi wa T-Mobile Arena Jijini Las Vegas nchini Marekani na kutetea taji lake la WBC uzito wa juu.
  Hiyo inakuwa mara ya pili mfululizo The Gypsy King anamchapa Bronze Bomber, baada ya kumdunda pia kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba Februari 22, mwaka jana ukumbi wa MGM Grand, hapo hapo Las Vegas.
  Pamoja na ushindi huo, Fury alikalishwa chini mara mbili na Bronze Bomber, lakini alisimama imara naye akamkalisha pia mpinzani wake huyo mara mbili kabla ya kummaliza raundi ya 11.
  Deontay Wilder akiwa chini baada ya kuangushwa na Tyson Fury raundi ya tatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Pambano la kwanza kabisa, wawili hao ambao wote wanapigana mtindo wa Orthodox, walitoka droo Desemba 1, 2018 ukumbi wa Staples Center, hapo hapo Los Angeles.
  Hilo linakuwa la 31 kwa Tyson Fury akishinda kwa mara ya 31 na kutoka sare moja, wakati Wilder amepoteza pambano la pili leo kwa mtu yule yule akibaki na rekodi ya ushindi wa mapambano 42 na droo moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY AMTWANGA TENA WILDER KWA KO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top