• HABARI MPYA

  Sunday, October 03, 2021

  SARE ZATAWALA LIGI KUU BARA LEO


  MECHI zote za Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo zimemalizika kwa sare za aina tatu tofauti. 
  Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wenyeji Namungo FC wamefungana 1-1 na Kagera Sugar ya Bukoba mkoani Kagera.
  Bao la Namungo FC leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Relliant Lusajo dakika ya  53, kabla ya mshambuliaji mwingine, Mbaraka Yussuf kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 71.
  Na Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Mbeya City wamefungana 2-2 na wapinzani wao wa Jiji, Mbeya Kwanza.
  Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 44 na Richardson Ng’ondya dakika ya 75, wakati ya Mbeya Kwanza yamefungwa na Crispin Ngushi yote dakika ya 77 na 88.
  Nao Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARE ZATAWALA LIGI KUU BARA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top