• HABARI MPYA

  Thursday, October 14, 2021

  CHAMA KUWANIA UCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA


  ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Mzambia Clatous Chota Chama ambaye kwa sasa anachezea RS Berkane ya Morocco atawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita.
  Chama atawania tuzo hiyo dhidi ya nyota wa Yanga, viungo pia Mkongo Tonombe Mukoko na Mzanzibari, Feisal Salum ' Fei Toto' katika hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA KUWANIA UCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top