• HABARI MPYA

  Wednesday, October 20, 2021

  MAN CITY YASHINDA 5-1 UBELGIJI


  TIMU ya Manchester City imewatandika wenyeji Club Brugge mabao 5-1 katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Jan Breydelstadion Jijini Brugge, Ubelgiji.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Joao Cancelo dakika ya 30, Riyad Mahrez mawili dakika ya 43 kwa penalti na 84 akimalizia pasi ya Fernandinho, Kyle Walker dakika ya 53 na Cole Palmer dakika ya 67, wakati la Club Brugge limefungwa na Hans Vanaken dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi sita baada ya mechi tatu na kupanda kileleni ikiizidi pointi mbili Paris Saint-Germain ambayo hata hivyo imecheza mechi mbili, wakati Club Brugge inabaki na pointi nne baada ya mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YASHINDA 5-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top