• HABARI MPYA

  Monday, October 18, 2021

  UFM KUTANGAZA MECHI LIGI KUU


  KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imeingia mkataba na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambao utairuhusu UFM 107.3 inayomilikiwa na Azam Media kurusha matangazo ya mechi zote za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Makabidhiano ya mkataba huo yamefanywa na Meneja Mwandamizi wa UFM, Baruan Muhuza na Meneja Masoko wa TBC, Fadhili Chilumba, kwenye ofisi za TBC Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa Muhuza, mkataba huu unaanza leo Oktoba 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFM KUTANGAZA MECHI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top