• HABARI MPYA

  Tuesday, October 19, 2021

  FEI TOTO AWAPA RAHA YANGA SONGEA


  VIGOGO, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwalaza wenyeji, wahamiaji KMC mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo wa kimataifa nchini, Feisal Salum Abdallah aliyefunga mabao yote mawili mapema kipindi cha kwanza na kuifanya timu ya kocha Mtunisia, Nasreddine Nabi anayesaidiwa kazi na Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi tisa baada ya mechi tatu za awali, mbili ikicheza ugenini.
  Fei Toto, alifunga bao kwanza dakika ya tano baada ya kufumua shuti kali lililombabatiza mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele kufuatia kudondoshewa mpira na kiungo mwingine, Mkongo Yannick Bangala aliyeuzuia mpira uliookolewa na mchezaji wa KMC.
  Mzanzibari huyo akafunga bao la pili dakika ya 12 kwa shuti kali pia la umbali wa mita mita 25 baada ya kutengewa pasi na Mayele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO AWAPA RAHA YANGA SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top